MASACHE KASAKA AWATEMBELEA WANANCHI ITUMBI AWASHUKURU AWATIA MOYO KUSAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO HUDUMA ZA KIJAMII
Akiwa
kijijini hapo Mheshimiwa Kasaka amekutana na makundi mbalimbali ya watu
wakiwemo wachimbaji wadogo wadogo ambapo ameahidi kufuatilia kero zao ili
ziweze kutatuliwa.
Amesema Kijiji cha Itumbi ni kati ya vijiji vyenye wachimbaji wengi wa dhahabu ambako kuna changamoto nyingi za huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu ambapo kwa kutumia ushirikishwaji wa wadau atajitahidi changamoto hizo zitapungua.
Aidha
amesisitiza wananchi na wachimbaji wadogo kuendelea kuiamini serikali ya awamu
ya tano ya Dkt John Pombe Magufuli ambayo imedhamiria kwa dhati kusaidia wanyonge
katika maeneo mbalimbali yenye changamoto.
0 Comments
Post a Comment