Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapongeza viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga kutokana na usimamizi mzuri wa Ilani ya CCM.

Amesema CCM imekuwa na ikitoa ushirikiano mzuri kwa Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini RUWASA kutokana usimamizi mzuri wa miradi ya Maji vijijini.

Amesema Wizara ya Maji itaendelea kutekeleza vyema ilani ya chama kinachotawala hususani katika kusimamia kwa karibu miradi yake ili kusaidia kupunguza kero za maji kote nchini.

‘’Tumedhamiria kwa dhati kabisa kumtua Ndoo Maji Mama Kichwani, tumejipanga kauli mbiu yetu ya Maji Bombani inatimia katika serikali ya awamu ya tano’’amesema Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca.