MHANDISI MARYPRISCA AWAFUTA MACHOZI MAHABUSU NA WAFUNGWA WANAWAKE GEREZA LA RUANDA MBEYA
Hatimaye machozi ya Mahabusu na
Wafungwa wanawake wapatao 38 na Mtoto mmoja waliopo katika gereza la Mahabusu
la Ruanda Jijini Mbeya yaanza kufutwa.
Mahabusu hao walitoa kilio chao mbele
ya Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi aliyeambatana na Mbunge wa
Jimbo la Mbeya Mjini Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dkt Tulia
Ackson ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani.
Kilio cha Mahabusu mbele ya Naibu
Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ilikuwa ni pamoja na nafasi finyu ya
Mabweni ya kulala sanjari na huduma za kijamii ambazo Mahabusu hao hujitegemea
kwa kuuza bidhaa mbalimbali wanazotengeneza kwa mikono yao.
Akizungumza jana mara baada ya
kutembelea gereza la Mahabusu Wanawake la Ruanda, Mhandisi Maryprisca aliahidi
kutatua baadhi ya changamoto ikiwa ni pamoja na kununua magodoro 10 kwa ajili
ya Mahabusu na Wafungwa gerezani hapo.
Akishukuru baada ya kupokea msaada
huo wa magodoro 10 kutoka kwa Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi
Mkuu wa gereza la Mahabusu Wanawake Mrakibu Mwandamizi wa Magareza Rehema Mwailunga
amewataka wadau wengine kujitolea kwa moyo kusaidia mahitaji ya mahabusu na
wafungwa wa gereza hilo.
0 Comments
Post a Comment