Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amewahakikishia wakazi wa Kata ya Kipapa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma kuwa Wizara ya Maji itaendelea kutoa fedha kugharimia m iradi ya Maji iliyoanza kutekelezwa maeneo mbalimbali nchini.

 
Akikagua mradi wa Maji uliopo katika kijiji cha Kipapa unaotekelezwa  na  Wakala wa Maji Vijijini RUWASA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Songea(SOUWASA) amesema ameridhishwa na kazi nzuri ambayo iko katika viwango vyenye ubora.

Pia Mhandisi Mahundi matumizi ya fedha za mradi zinazotolewa zinafanya kazi inayostahiki na kwamba kukamilika miradi inayotekelezwa na serikali kutasaidia kuondoa kero za wananchi wa kata ya Kipapa na wale wanaoishi jirani na kata hiyo.

Amesema mradi huo wa maji wa Kipapa  na miradi mingine inayojengwa kwenye vijiji mbalimbali itaondoa kero ya wananchi kutembea mbali kutafuta maji nah ii ndio lengo halisi la serikali la Kumtua Mama Ndoo Kichwani  na hivyo kuchochea uchumi wa Taifa.

Naye Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Songea Jafari Yahaya amesema mradi wa Maji wa Kipapa na Mhilo umeanza kutekelezwa Januari 2020 na kukamilika Marchi 2021 ambao umegharimu jumla ya Shilingi Mil 574 ambapo usanifu wa mradi ulitarajiwa kutumia Milioni 772.6 na kwamba fedha iliyobaki itatumika kutekeleza miradi mingine.