TUPONILE KOMBA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA ARUSHA"NYIMBO ZAKE ZATOA FARAJA"
"Tuponile
Komba ni mnyakyusa ila nimeolewa na Mngoni natokea Tukuyu Lutengano Kijiji Cha Igalamu nimelelewa Bulyaga Mpindo nimesoma shule ya msingi Bulyaga na sekondari Lutengano"ni kauli ya Tuponile Komba.
Ailianza huduma ya uimbaji akiwa mdogo wa miaka mitano aliimba shule ya jumapili makanisani umri ulipoendelea aliendelea kuimba kwaya mbalimbali ndipo akajua an kipawa cha uimbaji alianza kuimba binafsi mwaka 2015 .
"Nilitoa albamu ya kwanza ilibariki sana watu iliitwa Baba ninasogea msalabani na hata sasa makanisani huwa wanautumia kama wimbo wa kuabudu"alisisitiza Tuponile.
Mwaka2017 alitoa albamu ya pili iliyo gusa jamiii sana albam hiyo ilitwa Kesho yako inakuja na mwaka2020 alitoa albamu ya tatu inayo kwenda kwa kicheko changu Bwana ananifanyia ndani yake kuna Onjeni muone yakuwa Bwana yu mwema.
Tuponile ni mfanyakazi wa Serikali anajitahidi kupanga ratiba ili aweze kushiriki kote ingawa kuna wakati anakabiliwa na changamoto ila Mungu anamsaidia.
"Ninapokuwa kwa Kaisali navaa sura ya Ki kaisali na ninapokuwa kwa Jehovah nakuwa kwa Jehovah kweli, Oooh Mimi nina watoto watatu nawapenda sana"alisisitiza Komba.
Tuponile ameomba Watanzania kumuunga mkono katika huduma yake kwa kutembelea account zake za You Tube, Facebook, Instagram, Twitter kwa Jina Tuponile Komba waweze kuzitazama kazi zake na pia waweze kumuunga mkono pia kwa kupakua ili kazi ya Mungu isonge mbele mawasiliano yake ni 0752543439
0 Comments
Post a Comment