HABARI NJEMA
KWA WAKULIMA WA UFUTA WILAYA YA SONGWE
Baada ya
taharuki ya muda mrefu juu ya tija kwa wakulima wa bei ya Ufuta wilayani Songwe
mkoani Songwe hatimaye mnada mkubwa uliofanyika katika kijiji cha Chang’ombe
kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani Bei ya ufuta imepanda hadi kufikia Sh 2,291 kwa Kg 1 kutoka Sh 1,300 kwa Kg 1 ya awali kwa soko la Mbalizi.
Katika mnada
huo ambao umehudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah amesema kuwa
bei hiyo imefikia hatua hiyo baada ya wakulima kuukubali mfumo kupitia vyama
vya Ushirika AMCOS.
Amesema kuwa
AMCOS mbili zilipanga kufanyika kwa mnada huo katika kijiji cha Chang’ombe na
kupatikana kwa bei ya juu ya Ufuta ya Sh 2,291 kwa Kg 1 badala ya bei ya awali
ya mitaani ya Sh 1,300 Kg 1.
Jeremiah
amewataka wakulima kuuza ufuta kwa bei ya mtandaoni kwa soko la Kimataifa bila wakulima
kufahamiana ikiwa ni pamoja na kukusanya mazao yao ghalani ambako huko kuna uwezekano mkubwa wa kupata bei nzuri
kupitia soko la Kimataifa.
0 Comments
Post a Comment