WAKULIMA WA TUMBAKU CHUNYA WATINGA BUNGENI KUFUATILIA MADAI YA MSIMU ULIOPITA

*Ni USD 240,000 za Msimu wa Tumbaku 2020

Viongozi wa Vyama vya Ushirika AMCOS  kutoka Vijiji vya Lyeselo,Kalangali na Nkung’ungu Jimbo la Lupa wilayani Chunya wamefika Jijini Dodoma na kutembelea bungeni ambako wamefuatilia madai ya malipo ya Tumbaku msimu uliopita.

Fedha hizo ni Kiasi cha Dola za Kimarekani 240,000 za Msimu wa Tumbaku wa Mwaka 2020-2021

Pichani ni viongozi hao wa Vyama vya Ushirika wakiwa na Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe na Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Njelu Kasaka.