TANZANIA NA POLAND ZAKUBALIANA KUIMARISHA HUDUMA ZA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MAJIJI YA DAR NA DOM

Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Watu wa Poland zimeingia makubaliano ya kuimarisha huduma za maji na usafi wa mazingira katika majiji ya Dar es Salaam na Dodoma kupitia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miradi ya maji Taka Mji wa Kiserikali na kuongeza kiwango cha upatikanaji maji Jijini Dodoma na kupunguza upotevu wa maji Jijini Dar es salaam.

Akizungumza kwa Niaba ya Serikali ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania  Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa hatua hii  ni muhimu katika kuhakikisha Jiji la Dodoma linafikia  malengo kwa upatikanaji wa maji ya Uhakika.

Amesema kuwa jambo hili limekuwa muhimu zaidi kutoka na umuhimu wake hasusan  ikizingatiwa kuwa Jiji la Dodoma ndio makao makuu ya nchi linalokuwa kwa kasi na ongezeko la watu na makazi.

Mhandisi Mahundi amesema kuwa serikali imejizatiti barabara katika kukabiliana na upotevu wa maji katika Jiji la Kibiashara la Dar e Salaam na kuongeza kiwango cha makusanyo ya mapato na kudhibiti matumizi kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira(DAWASA).

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayesimamia Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Bara la Afrika na Afrika Mashariki ya Kati Mhe Pawel Jablonski amesema serikali ya Poland ipo tayari kutekeleza makubaliano kwa lengo la kuendeleza sekta ya maji nchini Tanzania na kuimarisha mahusiano ya nchi mbili hizi.

Kutoka Poland ujumbe umeongozwa na Mhe Powel Jabionski Balozi wa Poland nchini Tanzania Krzystol Buzailski na Maofisa Waandamizi kutoka nchini Poland.

Makubaliano hayo ni matokeo ya majadiliano ya  takribani  miaka mitatu tangu serikali hizo zilipokutana kwa lengo la kukuzana kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya maji nchini.