Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi,amewaagiza Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Babati (BAWASA)kuhakikisha ndani ya siku moja wanaweka Miundo mbinu ya maji kwenye chujio la maji la Mradi wa maji Darakuta-Magugu.

Mhandisi Maryprusca amesema kuwa mradi huo umetekelezwa vizuri kwa viwango vinavyostahili,hatua iliyobaki ni kuweka ni kuweka Miundo Mbinu na dawa jambo ambalo haliwezi kuchukua muda na gharama kubwa.

Amesema kuwa hiyo itasaidia kwa wakati huu ambapo wananchi wanahitaji wapate huduma ya maji wakati Mamlaka ikiendelea na mipango yake ya kutengeneza Miundo Mbinu bora nay a kisasa zaidi.

Mradi wa Maji wa Darakuta-Magugu unatekelezwa kwa zaidi ya Shilingi Bilioni 3 na utekelezaji wake uko kwenye hatua za mwisho, ukitarajia kuhudumia zaidi ya wananchi 80,000 wa mji wa Magugu.