MHANDISI MARYPRISCA AKUNJUA MAKUCHA
AAGIZA KUTUMBILIWA FUNDI WA MIUNDO MBINU.
Ziara ya Naibu Waziri wa Maji
Mhandisi Maryprisca Mahundi Mkoani Manyara imesababisha fundi wa Miundo mbinu Amos
Abi kukaa mguu nje mguu ndani.
Mhandisi Maryprisca amebaini hujuma
dhidi ya jitihada za serikali za kumtua Ndoo Mama Kichwani zikishindwa
kutekelezwa ipasavyo baada ya baadhi ya vituo kushindwa kutoa maji kutokana na
kutofanyiwa matengenezo.
Amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya
Babati Mhandisi Felix Mollel kumuondoa katika kazi fundi wa mradi wa Maji
katika kijiji cha Gidas Amos Abi.
Amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa
vitendea kazi fundi huyo hakuvifanyia kazi na kusababisha baadhi ya vituo vya
kuchotea maji kijijini hapo kushindwa kutoa huduma kwa wananchi.
Kadhalika Naibu Waziri wa Maji
Mhandisi Maryprisca ametoa siku tano kwa Meneja wa RUWASA Wilayani humo
kuhakikisha kasoro zilizobainika zinapatiwa utatuzi na maeneo yote yanapata
maji safi na salama.
Pia amewataka Wataalamu wa maji kote
nchini kutopendelea kukaa ofisini bali watembelee miradi ya maji ili kubaini
changamoto na kuzitatua.
0 Comments
Post a Comment