Mbio za Mwenge Maalumu wa Uhuru  unatarajia kuwekwa jiwe la Msingi Jumapili Sept 12,2021 kwenye mradi wa Mabwawa ya samaki ya Rahabu Fish Farm wenye thamani ya zaidi ya Sh Mil 170 uliopo kijiji cha Kikota kata ya Kiwira wilayani Rungwe mkoani Mbeya.


Akizungumza na Mbeya Yetu Tv Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Rahabu Logistics Limited Benjamin Mwandete amesema kuwa anatarajia kuongezea thamani mradi huo na kujenga Hoteli maalumu ya samaki.



‘’Hapa najenga ghorofa, patakuwa Hoteli,mteja atakuwa anavua samaki na kuandaliwa chakula na samaki fresh wanaovuliwa hapo hapo’’

Amesema kuwa mbali na kuongeza ajira kwa watu ambao wamefanyakazi kwenye mradi huo vijana watajifunza ufugaji bora wa samaki kupitia mradi huo.

Mwandete amebainisha kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambayo imetoa fursa ya uwekezaji kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini na kukuza uchumi wa Taifa.

Amesema gharama ya mradi huo kiasi cha Sh Mil 170 zimetokana na mkopo kutoka Benki ya AZANIA ambapo anaamini faida itapatikana kutokana na uhitaji wa samaki maeneo mengi hapa nchini.

‘’Mradi huu una jumla ya Mabwawa 21 wenye jumla ya vifaranga vya samaki elfu 24’’