MRADI WA MAJI SAFI WA MIL 600 KIJIJI CHA MAHEGE KIBITI KUANZA MWEZI AGOSTI.

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amezungumza na wananchi wa Kijiji cha Mahege Wilayani Kibiti mkoa wa Pwani na kuwapa uhakika wa utekelezwaji wa mradi wa maji eneo hilo kuondoa adha ya upatikanaji wa Maji Safi.

Mhandisi Maryprisca amesema kuwa Mwezi Agosti serikali itapeleka jumla ya Shilingi Milioni 100 ili kuanza rasmi utekelezaji wa mradi huo ambao Wakala wa Maji Vijijini RUWASA wamefuatilia na kubaini kwamba utagharimu jumla ya Shilingi Milioni 600.

‘’Wataalamu wameniambia kuwa utachukua miezi 6 kukamilika,miwatoe hofu, Rais Wetu Mama Samia amejipambanua kwamba Yeye ni ‘’Mama Maji’’ Hataki Kuona Akina Mama wa Kitanzania Wakihangaika kutafuta huduma ya Maji Safi na Salama’’ Amebainisha Mhandisi Maryprisca.