Waziri wa Ardhi William Lukuvi
akizindua Mpango wa Kitaifa wa Urasimishaji Makazi uliofanyika katika Kijiji
cha Igawa kata ya Igawa Wilayani Mbarali mkoani Mbeya, wengine katika picha
kutoka kushoto, ni Mkuu wa Wilaya Mbarali Reuben Mfune, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Juma Homera, ,Kaimu Mkaguzi mkuu wa ndani wa Benki ya NMB Benedicto Baragomwa Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi Mary Makondo, na Mkufunzi Chuo cha Ardhi Dkt Victoria
Mwakalinga.
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipongezana na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani
wa Benki ya NMB Benedicto Baragomwa mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa
wa Urasimishaji Makazi katika Kijiji cha Igawa Wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi William Lukuvi akiwa na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB
Benedicto Baragomwa wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wa Urasimishaji
Makazi, uzinduzi ambao umefanyika Kitaifa kata ya Igawa Wilayani Mbarali Mkoani
Mbeya. Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani ya Benki
ya NMB Benedicto Baragomwa akielezea mpango wa NMB wa kushirikiana na Wizara ya
Ardhi katika kuwawezesha Wananchi kufikia malengo ya umiliki wa ardhi wakati wa
Mpango wa uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wa Urasimishaji Makazi wilayani Mbarali
mkoani Mbeya. Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wakazi wa Kata ya Igawa
Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya(hawako pichani)umuhimu wa kurasimisha ardhi kwa
ajili ya maendeleo endelevu ya watu na Makazi. Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimnyanyua mkono Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma
Homera ikiwa ni ishara kukamilisha kwa uzinduzi wa mpango wa Kitaifa
urasimishaji makazi ambao umeanzia wilayani Mbarali mkoani Mbeya. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi William Lukuvi akimtambulisha Mkufunzi wa Chuo cha Ardhi Dkt Victoria
Mwakalinga wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wa Urasimishaji Makazi
uliofanyika wilayani Mbarali Mkoani Mbeya. Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimpa maelekezo Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani
wa Benki ya NMB mara baada ya kukamilisha uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wa
urasimishaji Makazi uliofanyika Igawa wilayani Mbarali mkoani Mbeya, wengine
katika picha ni Vicky Bishubo(NMB)Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Mary Makondo na
Mkufunzi wa Chuo cha Ardhi Dkt Victoria Mwakalinga.
0 Comments
Post a Comment