Mbunge wa jimbo la kavuu wilaya ya Mlele Mkoa wa katavi  Mh Geophrey Pinda 

 

  Mbunge wa jimbo la kavuu wilaya ya Mlele Mkoa wa katavi  Mh Geophrey Pinda   ametoa saa 72 kwa afisa biashara hlm ya mpimbwe kuwapa leseni wafanyabiashara ambao wamekwishalipia na agizo hilo limetolewa  baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wakidai ni miaka miwili sasa tangu walipie leseni na hawajakabidhiwa.


Mmoja wa wafanyabiashara anaefahamika kwa jina la Kadaso lutima ametoa malalamiko hayo kwenye kikao kilichohusisha watu mashuhuli katika mji mdogo wa kibiashara wa Majimoto ambapo wamemlalamikia afisa biashara kwa kuwasababishia kusumbuliwa na mamlaka mbalimbali wanaokwenda kukagua madukani kwao na kukuta hawana leseni z biashara.


“mkurugenzi kwani kuna ugumu gani afisa biashara kutupa leseni zetu tumeshalipa hela za leseni lakini anakuwa mgumu kutupa leseni zetu kwani kuna nini au hamna vitabu vya leseni Zaidi ya mwaka wa pili tunaendesha biashara bila leseni”


Nae mbunge wa jimbo hilo Mh Geophrey Pinda amemtaka afisa biashara huyo kuwakabidhi wafanyabiashara leseni ndani ya saa 72 na kumtaka ajipime kama ana weredi na nidhamu katika kazi yake.


“Natoa saa 72 wafanyabiashara wote waliolipia leseni wakabidhiwe,hawa niwatu wa kuwabembeleza maana wanaiingizia mapato halmashauri yetu,mkurugenzi huyo afisa biashara kama hawezi kazi weka pembeni mpe nafasi mtu anaeweza kuwahudumia wananchi”


Kwa upande wake mhasibu wa  hlm ya Mpimbwe bwana Masabiki Mashauri amesema hana taarifa ya wafanyabiashara hao kulipia fedha za leseni na kutokupewa na kuahidi ndani ya saa 72 atafatilia kwanini hawajapewa leseni na watapewa leseni zao.


“Mtu anapolipia leseni anapata leseni malalamiko niliyoyasikia nitayashughulikia haraka kujua nini tatizo mpaka hawajapewa leseni zao mpaka sasa”.


Afisa biasahara huyo alikimbia kikao licha ya kupewa taarifa siku moja kabla na wafanyabiashara walipotoa malalamiko hayo juhudi za kumtafta huku kikao kinaendelea hazikuzaa matunda.


         MWISHO